The gospel swahili

1 Zaidi ya hayo, ndugu zangu, nawaarifu ile injili niliyowahubiri, ambayo mliipokea na ambayo mnasimama ndani yake;
2 ambayo kwa hiyo mnaokolewa, ikiwa mnayashika maneno niliyowahubiria, isipokuwa mmeamini bure.
3 Kwa maana naliwatolea ninyi kwanza yale niliyoyapokea mimi mwenyewe, ya kwamba Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, kama yanenavyo maandiko;
4 na kwamba alizikwa, na kwamba alifufuka siku ya tatu, kama yanenavyo maandiko;